MANIFESTO YA JUMUIA YA VIJANA KWA KARNE YA 21. 1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.
Wakiwa wamealikwa na Bunge la Ufaransa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), Bunge la watoto duniani walikutana kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 21hadi 27Oktoba 1999 katika jiji la Paris. Mkutano huo ulihudhuriwa na watoto 350 toka katika nchi 175.
Katika mkesho wa mwaka 2000, mwaka uliotabgazwa na Umoja wa Mataifa kuwa mwaka wa kimataifa wa "utamaduni wa amani."Kila kijana alikuwa na shauku ya kutoa fasili yake kuhusu ulinzi wa amani, mshikamano, kuhusu elimu na utamaduni, maendeleo ya kiuchumi na ya kibinadamu na kuhusu kinga ya vyombo vya habari kwa kukubali azimio ya Manifesto ya Jumuia ya vijana kwa karne ya 21 ya tarehe 23 Oktoba 1999.
Manifesto hii inrasimisha izingatio wa vijana wa kanuni ambazo zilizowahi kuhamasishwa na Azimio la haki za binadamu na haki ya raia ya mwaka 1789 na Tamko la kimataifa kuhusu haki za binadamu la tarehe 10 Desemba mwaka 1948.
Manifesto hii ilipelekwa mbele ya ya Mkutano Mkuu wa UNESCO tarehe 26 Oktoba 1999. Ilani hiyo ya kanuni itapewa kwa watala na viongozi wa nchi mbalimbali, vile vile kwa Maspika wa mabunge, na mwanzoni wa mwaka 2000, itatangazwa rasmi kwa Umoja wa Mataifa.
Federico Mayor
Mkurugenzi Mkuu wa UnescoLaurent Fabius
Spika wa Bunge la Ufaransa
Maandiko ya Manifesto:
Sisi vijana toka katika nchi 175 tukiungana chini ya mwanvuli wa Bunge la watoto duniani tarehe 27 Oktoba 1999, tuliikubali Mnifesto ifuatayo:
1. AMANI NA KUTOTUMIA NGUVU. 2. ELIMU. 3. VYOMBO VYA HABARI. 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU. 5. MSHIKAMANO. 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI. 1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.
1.AMANI NA KUTOTUMIA NGUVU.
Sisi vijana wa karne ya 21, tunataka karne hii iwe ya amani miongoni mwa mataifa yote. Staarabu, tamaduni, na dini anuwai duniani zote zina lengo moja tu: kudumisha hali bora ya walimwengu na ulinzi wa amani. Hii ndiyo falsafa ya msingi ambayo mataifa yote yanatakiwa kutangaza. Ni vema kuchanganua yaliyopita ili kupata fundisho katika siku zijazo, lakini ni bora zaidi tujaribu kuondoa mminyano ama ukandamizaji wa wakati huu.
Dunia haina budi kuwania amani kwa njia za kidiplomasia, mazungumzo, juhudi za pamoja na kwa njia zingine zote zile mujarabu. Amani siyo ndoto bali ni lengo la kutimilika. Amani ni kilele ya kufikia, lau kana, Jumuia ya kimataifa itanuia hivyo na kuiendeleza. Kwa dunia nzima ni tumaini pekee ya kuendelea kuishi. Vita ni ugonjwa mbaya sana. Vita vilianzishwa na watawala vipofu, ambao walisahau kwamba kutokana na mipango yao ya kivita, walizima mustakabali wetu na dahari walizika chini ya magofu haki yetu ya kuishi na ya kuwa na siha. Miongoni mwa chanzo za vita viliorodheshwa ni mgao usiokuwa sawa wa mali, chuki zitokanazo na ubaguzi wa rangi, imani za kidini, kiitikadi, na kijinsia; utaifa potofu na ughaibu wa demokrasia na mifumo ya kiutawala ya kiimla.
Kutokana na hali hiyo tunapendekeza yafuatayo:
1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.
2. ELIMU.
Tupo katika mkesha wa karne ya 21.Elimu ndio ufunguo wetu. Tunatambua umuhimu wa elimu endelezi, unaofunguliwa kwa wote pasi ubaguzi wa rangi, wa kijinsia, pasi kuzingatia hali ya kiuchumi, imani za kidini ama ada za kimila.
Tunaamini kwamba elimu haiwahusu walimu na wanafunzi tu bali inahusu jamii nzima, ikimaanisha, wazazi, watawala wa umma, viongozi wa kidini, makampuni, mashirika isiyokuwa ya kiserikali na vyombo vya habari, na kwamba jumuia ya kimataifa haina budi kuleta mchango wake, wakati ukiitajika.
Tunamaizi kwamba elimu inaweza kutunufaisha yafuatao:
Tunapendekeza jumuia za kitaifa na za kimataifa zizingatie yafuatayo:
Tunapendekeza yafuatayo kwa viongozi wahusika:
Tutajitolea kufanya yafuatao:
1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.
3. VYOMBO VYA HABARI.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya binadamu, maendeleo yanaweza kuleta athari mbaya dhidi ya dunia, ambayo walimwengu hawakuwa wanatarajia: mabadiliko ya hali ya hewa, ajali za nyuklia, ufundi wa kijenetiki, kutoweka kwa wanyama na mimea.
Hata hivyo mahaluku anaendelea kuona hali hiyo kama hali ya kawaida, pasi kutafakari anaendelea kuwa mzalishaji na mtumiaji: uchafuzi unaotokana na viwanda, uharibifu wa mazingira, na kutokujali akiba ya mali asili hizo tukizingatia ongezeko la wakazi wa dunia unapanda kwa kasi, mali asili hiyo haitatosheleza watu wote, hali ambayo itakuwa kiini cha mizozo na vita.
Sisi vijana katika mkesha wa kikwi (milenia) ya tatu, kutokana na hali hiyo tunapendekeza yafuatao:
1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.
4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU.
Tunataka, mahitaji muhimu mathalani afya, elimu, chakula cha kutosha, kiwango cha maisha cha kuridhisha, kutoweka kwa ubaguzi wowote ule, vinatakiwa kuimarishwa.
Kuwania kilele cha mahitaji yale, hatuna budi kusitisha ama kuepukana na vyanzo vyote vya migogoro. Kilele cha himaya cha vipengee hivyo tulivyotaja hapo juu tunaweza kuifikia kwa njia hii: uhuru wa kujieleza ama wa kutoa maoni, kuimarisha mazingira ya uwazi, na kuheshimu imani ya kidini ya wengine. Viongozi wote wa kiserikali hawana budi kuwaadhibu wale wote ambao hawataheshimu haki hizi za aula.
Watawala wanatakiwa kuhimili mambo ya aula, wakizingatia uchunguzi wa hali ya sasa wanaweza kutambua ni vipi wanaweza kuepukana na mizozo mbalimbali bado yakiwa katika hali ya utungaji. Moja ya mambo ya aula yale ni kuandaa kampeni ya kimataifa dhidi ya utumiaji wa madawa ya kulevya, ambayo inaweza kusaidia kuhakikisha kupatikana kwa mustakabali bora kwa wakazi wote duniani. Uzazi wa mpango, usawa wa kinjisia, elimu, vipengee hivi ni mihimili ya mustakabali wa amani; vinatakiwa kuorodheshwa katika vipengee hivyo vya aula. Yote haya yanatakiwa kujumulishwa na dhamira wakfu ya hisia ya amani. Ingelikuwa vema zaidi kuhimili misingi ya kuepukana mapema na mizozo mbalimbali. Sisi, vijana, tunataka kujenga dunia ambamo watoto hawatafanywa askari, ugaidi na silaha za maangamizi makubwa vitatoweka.
Ili kupunguza makali ya matatizo yanayotokana na ujanja na riba kubwa inayotakiwa kulipwa na nchi zinazoendelea kwa nchi zilizoendelea, tunapendekeza kuundwe shirika ya kimataifa, ambayo itakuwa na dhima ya kusimamia mikopo na ulipaji, kupunguza riba kubwa inayotozwa na nchi zilizoendelea na kutoa msamaha wa madeni kwa zile nchi ambazo zinazoshindwa kulipa kutokana na matatizo mbalimbali. Ili kuepuka kutokuwepo na usawa wa nguvu baina ya mataifa, tunapendekeza ingelikuwa vizuri kuandaa usawa wa kiuchumi duniani kote kwa minajili ya kufikia usawa wa nguvu ya kiuchumi. Tunatakiwa kuimarisha usawa wa kiteknolojia kwa kufanya maarifa yetu yote kuwa mali ya pamoja.Ili kuepukana na migogoro mbalimbali, tunapendekeza kuimarishwe mawasiliano kati ya watawala na watawaliwa duniani kote.
1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.
5. MSHIKAMANO.
Kwa maoni yetu, mshikamano inamaanisha kuwathamini na kuwaheshimu wengine. Inamaanisha tena kuwasaidia wengine kama vile sote ni ndugu wa familia moja. Inabainisha kwamba: kuwatendea wengine kama vile tungelipenda watundee, na hakuna cha ziada cha kutarajia. Mshikamano inamaanisha kufanya kazi pamoja kwa kuzingatia malengo ya pamoja, kwa kujitolea au kushiriki katika agano la pamoja.
Ndio sababu sisi vijana tungelipenda kuwasaidia, kuwaheshimu, na kuwajali wanaohitaji msaada pasi kuangalia wanatoka wapi, ni wa mbari, utamaduni ama dini gani.
Ili kusukuma mbele gurudumu la mshikamano, tunaweza kutalii yafuatao:
1.AMANI NA KUTOKUTUMIA NGUVU - 2. ELIMU - 3. VYOMBO VYA HABARI - 4. MAENDELEO YA KIUCHUMI NA YA KIBINADAMU - 5. MSHIKAMANO - 6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.
6. UTAMADUNI, MAWASILIANO NA MABADILISHO YA MAWAZO KATI YA TAMADUNI TOFAUTI.
Wakati tunapofikia tamati ya karne ya 20, ni muhimu kuulinda utamaduni wetu, kujifunza kwa njia ya mawasiliano kuhusu tamaduni zingine, kushadidi tamaduni ya mabadilisho ya mawazo na maoni, na kurahisisha mawasiliano kwa manufaa ya amani na maendeleo madhubuti duniani kote.
Utamaduni unatupatia kitambulisho na hisia ya kuwepo kwetu.
Jamii zetu haraka sana zilipiga hatua kubwa ya maendeleo, kwa hivyo ni muhimu sana kwetu kuzilinda tamaduni zetu ili zisije zikatoweka.
Ndio sababu sisi vijana duniani kote tunatoa shime hii ili:
Vyombo vya habari lukuki, pamoja na njia za mawasiliano na teknolojia ya kisasa viliwawezesha vijana kujieleza sana na kuonesha hisia zao bayana. Ndio sababu njia za kisasa hizo zinatakiwa kupelekwa kwa vijana wote duniani kote.
Mfumo wa Umoja wa Mataifa unatakiwa uzindue kampeni kabambe baina ya mataifa kwa msaada wa nchi zilizoendelea mbalimbali wanachama wake na tawala za kanda, kampeni za kuwakabidhi vifaa muhimu : mdahalishi( internet ), wavuti( website ) maalum itakao wavutia vijana, na barua ya elektronikia (E-mail).
Tunapendekeza kwamba vijana na mashule zipunguziwe bei ya utumiaji na uunganishaji wa vyombo hivyo vya mawasiliano hususan mdahalishi.
Tungependa kuchapisha gazeti letu binafsi katika nyanja ya kitaifa na ya kimataifa na tungependa vile vile wazazi wetu na wengine wa makamu yao waweze kuisoma. Kwa sababu mawasiliano inaenda sambamba na ujuzi wa lugha, tunapendekeza, watawala wetu wapitishe sheria ambazo zitatuwezesha kujifunza lugha za kigeni pasi na vikwazo haraka iwezekanavyo, iwe mashuleni ama mahali pengine.
Historia na hali halisi ya sasa inatufundisha kwamba vita, mauaji kaumu ya kikabila na ubaguzi wowote ule na ukandamizaji vinaweza kuepukika kama tutaimarisha ubadilishaji wa mawazo wa kiutamaduni, kwa sababu zoezi hili linaweza kuimarisha uelewano kuhusu utamaduni wa watu wengine, heshima baina yetu na itawezesha kutowesha hisia za chuki zizokuwa na sababu yoyote na kuondoa hisia zingine zote zile za kizuzu kuhusu wengine.
Sisi vijana wa dunia nzima tunajitolea kuheshimu maoni na imani ya wengine.
Imafaima tunataka kufaidika na msaada wa UNESCO ili kuendeleza uhai wa Bunge la Watoto Duniani Kote na kulinda utamaduni wa nchi zote, wa makabila madogo madogo na makabila mengine ya kijadi.
Manifesto ya Jumuia ya Vijana kwa Karne ya 21, iliyopendekezwa na Bunge la Watoto Duniani kote walikutana katika Bunge la Ufaransa jijini Paris, ilikabidhiwa, mwishoni mwa mkutano huo tarehe 24 Oktoba 1999 kwa Mheshimiwa Spika wa Bunge la Ufaransa Laurent Fabius na kwa Mstahiki Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Federico Mayor ambao wote waliweka sahihi juu ya nakala mbili halisi ambazo zilikuwa katika lugha ya Kiingereza, Kihispania na Kifaransa.
( Kazi hii imetafsiriwa kwa Kiswahili toka katika lugha ya Kiesperanto na Mwalimu Matabaro Minani Semutwa mkazi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.)
enpaøigis : Daniel Durand